Mkombozi and CRDB Banks PLCs Announced 2016 Dividends due in 2017

Mkombozi Bank and CRDB Bank PLCs have announced dividends of Tshs. 20/- and Tshs. 10/- per share for this year, respectively. Zan Securities Chief Executive Officer, Mr Raphael Masumbuko speaking with ‘Daily News’ for Mkombozi Bank said that dividend proves that short short and long term investment pays. “Bank investors have started to reap their fruits of investments…  is a good gesture that even investing to no names listed firms pays,” Mr Masumbuko said.

Mkombozi Bank Chairman, Mr Method Kashonda said payment of dividend will be through bank accounts and mobile money platform such as M-pesa, Airtel Money, and Tigo-pesa. Mkombozi’s Managing Director, Mrs Edwina Lupembe said the bank had posted an impressive performance last year from its six branches country-wide.

Likewise, shareholders of CRDB Bank met in Arusha this month to endorse that Tshs. 10/- per share dividend proposed by the board April 13, 2017. The Tshs. 10/- per share translates into a total dividend of Tshs. 26 billion to be deducted from bank’s last year net profit of Tshs. 75 billion, the bank Managing Director, Mr Charles Kimei said. Pursuant to approval of the dividend recommendation, the timetable for dividend payment by the CRDB is scheduled to be on or about 2nd June 2017.

 

Benki za Mkombozi na CRDB zimetangaza gawio la sh. 20/- na sh. 10/- kwa kila hisa kwa mwaka huu, kila mojawapo. Afisa Mtendaji wa Zan Securities, Bw Raphael Masumbuko akiongea na gazeti la ‘Daily News’ kwa ajili ya benki ya Mkombozi alisema kuwa gawio lililotangazwa linathibitisha kwamba uwekezaji wa muda mfupi na mrefu unalipa. “Wawekezaji katika benki wameanza kuvuna matunda yao ya uwekezaji … ni ishara nzuri kwamba hata kuwekeza kwenye kampuni zenye majina madoko kwenye soko inalipa,” Bw Masumbuko, alisema.

Mwenyekiti wa benki ya Mkombozi, Bw Method Kashonda alisema kuwa malipo ya gawio yatafanyika kupitia akaunti za benki na kupitia akaunti za mitandao ya simu za mkononi kama vile M-pesa, Airtel Money, na Tigo-pesa. Mkurugenzi Mtendaji wa Mkombozi, Bi Edwina Lupembe alisema kuwa benki ya Mkombozi imekuwa na utendaji mzuri na wa kuvutia zaidi mwaka jana katika matawi yake sita nchi nzima.

Vivyo hivyo, wawekezaji wa benki ya CRDB walikutana Arusha mapema mwezi huu kuidhinisha gawio la sh. 10/- kwa kila hisa mgao uliopendekezwa na bodi ya CRDB Aprili 13, 2017. Kiasi hicho cha gawio la sh. 10/- kwa kila hisa kinatokana na jumla ya mgao wa sh. bilioni 26 unaotokana na faida ya sh. bilioni 75 za benki ya CRDB iliyopata katika kipindi cha mwaka jana, Mkurugenzi Mkuu, Bw Charles Kimei alisema. Kwa mujibu wa idhini na mapendekezo ya gawio, ratiba ya gawio la benki ya CRDB imepangwa kufanyika Juni 2, 2017 au muda mfupi baada ya hapo.

#Mkombozi Bank   #CRDB Bank

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *