Biashara ya nafaka katika kanda ya Afrika Mashariki inatarajiwa kuongezeka kufuatia kuimarishwa kwa Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika viwango vya vyakula vikuu 2017.
Wadau wa mnyororo wa thamani, chini ya Uongozi wa Baraza la Mazao la Afrika Mashariki (EAGC), hivi karibuni jijini Nairobi walizindua viwango 11 vilivyobuniwa kwa minajili ya vyakula vikuu, sampuli na njia za upimaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa EAGC, Gerald Masila anasema kufuatia uimarishwaji wa maombi ya matumizi ya viwango, wakulima watafikia masoko bora na makubwa, wakati watumiaji watafurahia bidhaa bora na salama za nafaka.
Makubaliano ya uimarishwaji wa viwango hivyo ambavyo vinatarajiwa kuridhiwa ndani ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, yalizinduliwa na kuwasilishwa kwa utekelezaji wakati wa kumalizika kwa Mkutano wa mwisho wa mwaka wa Wanachama wa EAGC uliofanyika jijini Nairobi mwezi uliopita.
Katibu Mkuu wa EAC, Betty Maina alisema viwango vya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kwa nafaka na jamii ya kunde vilitangazwa rasmi na EAC mwaka 2013.
Lakini, kwa viwango Maina alisema, haviwezi kutekelezwa ili kutambua muundo wa biashara ya nafaka ndani ya kanda kutokana na vikwazo kama vile mahitaji ya usalama na ubora, sampuli na njia za upimaji.
“Mapungufu yaliyopo yanahitaji mapitio, mchakato ambao umekwisha kufikia viwango vya mwaka 2017 vinavyokubalika na Jumuiya,” aliongeza.
Viwango tisa vya kipaumbele vya bidhaa vilivyopitiwa ni mahindi, ngano, mchele, maharage, soya, unga wa mahindi, unga wa ngano, unga wa mtama na unga wa ulezi.
Baadhi ya vigezo vilivyozingatiwa kwa njia ya marekebisho ya viwango vilikuwa viwango vya maudhui ya unyevu, utolewaji rangi nafaka, mazao sumu, miongoni mwa mengineyo.
Baraza la Mazao la Afrika Mashariki (EAGC), kwa msaada kutoka kwa washirika wa Maendeleo pamoja na Mashirika ya Maendeleo ya Kimataifa, SIDA, USAID, DFID, CTA, miongoni mwao; yamekuwa yakishirikiana na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) katika mchakato wa kuimarisha viwango vya mazao ya nafaka, mazao ya jamii ya kunde, na mazao mengine tangu mwaka 2010 na Baraza limehamasisha na kujitolea rasilimali na ushirikishaji wadau katika mchakato huu.
Taarifa Zaidi EA grain trade to intensify following standards harmonisation