Kenya na Tanzania zakubaliana kutatua vikwazo vya kibiashara

Na Mohamed Ahmed                                                                                                          January 31, 2018                                                                                                                                                                                    Kenya na Tanzania zimekubaliana kuondoa tofauti zao na kuanza kushughulikia kutatua vikwazo vya kibiashara kati ya nchi hizi mbili.

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa mjini Mombasa, nchi hizo mbili zitatoa ripoti yao Alhamisi kuhusu makubaliano ya kuondoa vikwazo visivyo vya kodi ili kuongeza biashara ya ndani ya kikanda.

Katibu Mkuu wa Biashara ya Kimataifa Chris Kiptoo na Mwenzake wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa Tanzania, Elisante ole Gabriel katika Mkutano wao uliofanyika katika Hoteli ya Sarova Whitesands, wamekubaliana kuondoa mikwamo ya kibiashara ambayo imetishia uhusiano mzuri kati ya nchi hizi mbili jirani.

Wamesema nchi hizi mbili zimekubaliana kuruhusu uagizaji na usafirishaji wa bidhaa kati yao.

“Tayari tumeweza kutatua usafirishaji wa ngano, maziwa na bidhaa za LPG. Zote hizi sasa zinasafirishwa kupitia mipaka bila tatizo lolote. Ili kuhakikisha kwamba tunaboresha biashara yetu ya kikanda tumeamua kuwa tutaondoa vikwazo, “Dr Kiptoo alisema.

MPANGILIO

Kutakuwa na tume ya kuthibitisha katika mpangilio maalum ili makubaliano kuwa ya mafanikio.

Dr Kiptoo alisema mazungumzo haya yaliyofanywa na wawakilishi wa nchi hizi mbili wamekubaliana kuwa na mikakati ya majadiliano ili kuboresha usafirishaji wa bidhaa.

“Tumekubaliana pia kuwa tuwe tukiwatembelea wananchi katika mipaka yetu na kutatua baadhi ya matatizo ambayo wanayo ili kuboresha mazingira ya kibiashara kati ya nchi zetu mbili,” aliongeza.

Prof Gabriel alisema mataifa haya mawili yataondosha “kodi zisizohitajika” za bidhaa.

Aliongeza kuwa Kenya na Tanzania watakuwa na mpango-kazi wa kutatua changamoto zinazowakabili katika biashara.

KUTOKUKUBALIANA

“Katika kila serikali lazima pawepo na kutokukubaliana lakini hatutaki tofauti zisizo na msingi amabazo zinaweza kutatuliwa.

Tuko katika mpango wa kuboresha viwanda vyetu na kukubaliana kufanya raia wetu kuendeleza maslahi ya kitaifa,” alisema Prof Gabriel.

Tofauti hizi mbili za hivi karibuni zilizotokana na mnada wa ng’ombe zaidi ya 10,000 na uchomaji wa vifaranga 6,400 vya Kenya na mamlaka za Tanzania.

MASUALA MADOGO

Dk Kiptoo amechukulia uamuzi wa serikali ya Tanzania kama “masuala madogo ambayo hayapaswi kupewa umaarufu mkubwa” na kuongeza kuwa “nchi hizo mbili zinayashughulikia vizuri”.

“Tumeona biashara kati ya nchi hizi mbili ikiboreka. Uhusiano kati ya Tanzania na Kenya ni mzuri na tunafanya vyema, “alisema.

Hata hivyo, alikubali kuwa katika miaka mitatu iliyopita, biashara kati ya nchi hizo mbili imepungua.

Kwa sababu hiyo, alisema, wanajitahidi kuona uwekezaji zaidi katika kila nchi kukua hususan katika bidhaa za kilimo na biashara.

“Tumejiuliza kwa nini biashara inapungua kati ya nchi zetu mbili na ni nani anayechukua sehemu kubwa ya biashara hiyo na tunafanyia kazi njia bora zaidi zinazofaa kushughulikia yote hayo,” alisema Dr Kiptoo.

More Info Kenya and Tanzania agree to resolve trade barriers

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *