LONDON, Uingereza
Thamani ya hisa za kampuni ya Petra Diamonds zaanguka baada ya Serikali ya Tanzania kukamata furushi lenye vipande vya almasi zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 15 (takribani sh. bilioni 33) kama sehemu ya Uchunguzi wa Kamati ya Bunge katika madai ya uhalifu katika Sekta ya Almasi.
Kampuni hii iliyoorodheshwa kwenye Soko la Hisa na Dhamana la London imelazimika kufunga mgodi wake wa Williamson, chanzo cha mawe haya, kwa kuwa “wafanyakazi wake muhimu” wanasaidia mamlaka kwa uchunguzi kuangalia jinsi almasi zinavyothaminishwa.
Hisa za kampuni hiyo, ambayo inasema “haijapewa taarifa rasmi” za sababu ya uchunguzi, zimeanguka kwa karibu asilimia 25% wakati soko lilipofunguliwa, kabla ya kurejesha thamani kwa asilia 6% chini, chini ya senti za kiingereza 6.2p kufikia senti 83.75p.
Almasi zilikamatwa uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam tarehe 31 Agosti wakati zikitayarishwa kusafirishwa kwa mauzo jijini Antwerp, na maafisa wa Tanzania wakidai kutothaminishwa ipasavyo.
“Wakati Kampuni Almasi ya Williamson katika nyaraka zake kuonyesha kwamba thamani ya almasi hizo ni dola za kimarekani milioni 14.798, uthamini mpya uliofanywa na serikali umeonyesha kuwa thamani halisi ya almasi hizo ni dola za kimarekani milioni 29.5,” ilisema taarifa ya Wizara ya Fedha.
“Miongoni mwa hatua za kisheria zitakazochukuliwa ni pamoja na kutaifishwa kwa almasi hizo zilizokamatwa baada ya kuthibitika kuwepo udanganyifu uliohusishwa katika kuonyesha thamani halisi ya madini hayo.”
Tanzania imeingia mtafaruku na makampuni kadhaa ya madini ya kigeni tangu uchaguzi wa 2015 wa John Magufuli, ambaye ni Rais anaejaribu kwa nchi kupata faida ya thamani itokanayo na mali ghafi.
Serikali yake juma lililopita iligundua “makosa” katika mchakato wa hisa za serikali katika Mgodi wa Williamson uliopunguzwa kutoka 50% hadi 25%, wakati pia Magufuli alishatoa agizo la uchunguzi juu ya madai ya uthaminishwaji wa chini kwa mauzo ya almasi nje.
Kampuni ya Petra inasema haijafahamishwa rasmi sababu za uchunguzi, ingawa ilitoa nyaraka kadhaa zinazohusiana na mchakato wa uthaminishwaji na malipo kwa serikali ya Tanzania.
Kampuni hiyo imesema kuwa usafirishaji wa karati za almasi 71,645 ulipewa thamani ya awali wa karibu dola milioni 14.8 na Shirika la Uthamini wa Almasi na Vito kabla ya kuandaliwa kwa kusafirishwa nje kwa mauzo.
Nyaraka za malipo ya mrabaha kwa serikali inaonyesha malipo ya karibu dola za kimarekani 888,000 pamoja na ada ya “ukaguzi na usafirishaji” ya karibu dola za kimarekani 150,000.
Kampuni hiyo pia imesema kuwa jumla ya malipo kwa serikali inategemea kile kilichopatikana kutokana na mauzo ya vito hivyo huko Antwerp, badala ya huo uthamini wa awali.
“Utaratibu wa ushindani wa wazi kwa kandarasi unaofanywa na kampuni ya Petra pia hutumiwa na makampuni mengine ya almasi na ina rekodi iliyothibitishwa ya uwazi katika bei,” kampuni hiyo ilisema.
“kampuni ya Petra ipo tayari kushirikiana na serikali ili kutatua suala hili na kuhakikisha kwamba taarifa sahihi zinapatikana kwa pande zote.”
“Kampuni itakuwa na fursa ya kuyashughulikia masuala mengine yote yaliyoibuliwa na matokeo ya Uchunguzi wa kamati ya Bunge mara itakapopokea nakala ya ripoti.”
Kampuni imesema shughuli za madini “zinafanyika kwa uwazi na kwa kufuata sheria kamili za Tanzania na Mchakato wa Makubaliano ya Kimberley”.
“Serikali ina fursa kamili ya uangalizi wa almasi zinazozalishwa katika mgodi, ambao hudhibitiwa na wawakilishi kadhaa wa serikali kwa kushirikiana na kampuni tangu hatua ya upatikanaji hadi hatua ya uuzwaji.”
Taarifa Zaidi: Petra Diamonds market value falls after Tanzania seizes $15m shipment