- Shirika lililosajiliwa Toronto, Tanzanian Royalty Exploration (CN: TNX) limemshukuru Rais John Magufuli, kwa kusema kuwa uwazi anaohitaji Rais katika sekta ya rasilimali, “ni wito ulio wazi kwa taratibu za pande zote kunufaika, na sio kutaifisha”.
Tanzania hivi karibuni ilipitisha sheria mpya zilizotungwa ili kuongeza mapato na kuipa uwezo serikali wa kufuta mikataba mibovu na kudhibiti usuluhishi wa kimataifa.
Mbali na sheria mpya, serikali imezuia mauzo ya makinikia ya dhahabu na shaba, ambapo uamuzi umesababisha kampuni ya Acacia Mining (LN: ACA) kutozwa malimbikizo ya kodi na penati zake mpaka kufikia dola za Kimarekani bilioni 190 katika migogoro na mchimbaji huyo, na mwezi uliopita ilitaifisha zaidi ya katati 70,000 za almasi kutoka mgodi wa Williamson unaomilikiwa kwa pamoja na Petra Diamonds (LN: PDL).
Hata hivyo Tanzanian Royalty Exploration, ambayo ina umiliki wa asilimia 45% ya mali na mapato ya mradi wa dhahabu wa Buckreef na serikali ya Tanzania, imesema kampuni zinazozalisha malighafi za madini zinapaswa kuwa na usawia katika kugawana mapato na serikali.
“Kama mfanyabiashara ninaefanya kazi nchini Tanzania kwa zaidi ya miaka 20, ni maoni yangu kwamba kufanya kazi kwa imani nzuri ni muhimu nchini Tanzania kama ilivyo kila mahali,” mwenyekiti mtendaji huyo, James Sinclair alisema.
“Rais Magufuli ni Kiongozi kwa wakati huu, nchini na barani.”
Alisema kampuni hiyo haikuathiriwa na sheria mpya na anatoa maoni ya hivi karibuni kuhusu msemaji wa serikali, ambaye alisema hakuna ukweli katika ripoti zinazodai kwamba nchi ilikuwa na mikakati kutaifisha miliki za migodi.
Kampuni hiyo pia ilianza mazungumzo na serikali mwezi Julai ili kufadhili mradi wa kisasa gravity/CIL katika mgodi wa dhahabu wa wazi (open pit) wa Buckreef ambao una uwezo wa rasilimali zaidi ya ounces milioni 1 ardhini.
Kwa Taarifa Zaidi: “President Magufuli is a man for this time, country and continent”