Barrick yakubaliana na Tanzania pia kutatua tatizo la kodi

Dar es Salaam/Toronto

Barrick Gold (ABX.TO) imesema Alhamisi hii kuwa kampuni inayoimiliki, Acacia Mining (ACAA.L) italipa dola za Marekani milioni 300 (paundi milioni 228.07 za Uingereza) na kugawana ‘faida za kiuchumi’ katika shughuli zake nchini Tanzania katika mpango wa makubaliano yaliyopendekezwa ili kutatua miezi miwili ya mgogoro wake na serikali ya Tanzania.

Mapema Alhamisi, Mwenyekiti wa Barrick, John Thornton aliuambia mkutano wa habari jijini Dar es Salaam kuwa kampuni hiyo imekubali kuilipa Tanzania dola za kimarekani milioni 300 kama ishara ya imani nzuri. Ilifafanua taarifa hiyo baadaye kuwa kampuni yake tanzu, Acacia itafanya malipo hayo.

Tanzania pia itapata sehemu ya asilimia 16 katika migodi mitatu ya dhahabu ya Acacia chini ya makubaliano hayo kwa mujibu wa Barrick na waziri wa serikali ya Tanzania. Acacia imesema imepokea nakala ya mpango wa makubaliano na itautolea ufafanuzi.

Thornton amesema makubaliano hayo yatahitaji idhini ya wanahisa huru wa bodi ya wakurugenzi wa Acacia. Bodi ya wanachama saba ya Acacia ina wakurugenzi wawili kutoka Barrick, mmoja kutoka Acacia na wakurugenzi huru wanne.

Serikali kutoka Indonesia hadi Afrika Kusini zinahitaji udhibiti mkubwa juu ya utajiri wa madini kwa jinsi bei za metali zinavyoongezeka. Baada ya kuhamia katika nchi zenye athari zaidi katika uchimbaji mpya, makampuni ya madini yanakabiliwa na kuongezeka kwa kile kinachoitwa utaifa wa rasilimali.

Barrick, kampuni kubwa duniani ya uchimbaji dhahabu inayomiliki asilimia 63.9 ya Acacia, ilianza mazungumzo na Tanzania mwezi Juni. Serikali ilipiga marufuku mauzo ya madini yasiyochakatwa na kutunga sheria mpya mapema mwaka 2017 ili kuongeza umiliki wa serikali katika migodi.

Acacia mwezi Julai ilipelekewa madai ya kodi za dola za kimarekani bilioni 190 kwa malimbikizo, adhabu na riba. Imekuwa ikituhumiwa na Tanzania kwa ukwepaji wa kodi kwa miaka kadhaa na pia kwa uthamini hafifu wa mauzo yake nje.

Ikiwa kampuni iliyosajiliwa kwenye soko la hisa la Uingereza, hisa za Acacia kwa siku ya Alhamisi zimefungwa zikiwa juu kwa asilimia 16 zikionyesha ahueni waliyopata wawekezaji wake katika makubaliano haya, wachambuzi walisema. Na hisa za Barrick zimefungwa zikiwa chini kwa senti 1 za Kanada kufikia dola za Kanada 20.15.

“Maelezo zaidi na ufafanuzi wa ziada unahitajika kuchunguza kikamilifu athari zake, lakini hadidu za makubaliano zinaonyesha kuwa na athari kidogo tofauti na matarajio,” alisema mchambuzi wa Masoko ya Hisa na Mitaji wa BMO,  Andrew Kaip katika taarifa yake ya Alhamisi.

Marufuku ya kusafirisha nje ilikuwa sehemu ya kushinikiza kwa ujenzi wa kinu cha uchenjuaji (smelter) nchini ili kufanya mauzo ya dhahabu ya nchi kuwa muhimu zaidi.

Rais John Magufuli hakusema kama marufuku ya kusafirisha nje ya nchi yataondolewa. Barrick na serikali itaunda kamati itakayofanyia kazi utatuzi wa madai ya kodi kwa Acacia.

“Kwa kuwa sisi sote ni wanahisa, tunaweza kukaa chini kwa kikombe cha kahawa na tukaamua masuala yoyote yaliyo bora,” Rais Magufuli alisema kwenye televisheni.

Pia aliamuru viongozi wa serikali kuanza mara moja majadiliano na wachimbaji wa almasi na tanzanite kufikia makubaliano kama hayo.

Tanzania ni wazalishaji wa dhahabu wa nne wa ukubwa barani na Acacia ni mchimbaji wake mkubwa zaidi.

Wiki iliyopita, Barrick ilisema uzalishaji wa robo ya tatu ya mwaka ulipungua kwa sababu ya masuala ya Tanzania.

Taarifa Zaidi: Barrick Gold, Tanzania reach partnership deal

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *