Category Archives: DSE Stocks/Shares, Infrastructure, Corporate and Municipal Bonds

Biashara ya nafaka EA kuimarika kufuatia Makubaliano

Biashara ya nafaka katika kanda ya Afrika Mashariki inatarajiwa kuongezeka kufuatia kuimarishwa kwa Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika viwango vya vyakula vikuu 2017.

Wadau wa mnyororo wa thamani, chini ya Uongozi wa Baraza la Mazao la Afrika Mashariki (EAGC), hivi karibuni jijini Nairobi walizindua viwango 11 vilivyobuniwa kwa minajili ya vyakula vikuu, sampuli na njia za upimaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa EAGC, Gerald Masila anasema kufuatia uimarishwaji wa maombi ya matumizi ya viwango, wakulima watafikia masoko bora na makubwa, wakati watumiaji watafurahia bidhaa bora na salama za nafaka.

Makubaliano ya uimarishwaji wa viwango hivyo ambavyo vinatarajiwa kuridhiwa ndani ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, yalizinduliwa na kuwasilishwa kwa utekelezaji wakati wa kumalizika kwa Mkutano wa mwisho wa mwaka wa Wanachama wa EAGC uliofanyika jijini Nairobi mwezi uliopita.

Katibu Mkuu wa EAC, Betty Maina alisema viwango vya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kwa nafaka na jamii ya kunde vilitangazwa rasmi na EAC mwaka 2013.

Lakini, kwa viwango Maina alisema, haviwezi kutekelezwa ili kutambua muundo wa biashara ya nafaka ndani ya kanda kutokana na vikwazo kama vile mahitaji ya usalama na ubora, sampuli na njia za upimaji.

“Mapungufu yaliyopo yanahitaji mapitio, mchakato ambao umekwisha kufikia viwango vya mwaka 2017 vinavyokubalika na Jumuiya,” aliongeza.

Viwango tisa vya kipaumbele vya bidhaa vilivyopitiwa ni mahindi, ngano, mchele, maharage, soya, unga wa mahindi, unga wa ngano, unga wa mtama na unga wa ulezi.

Baadhi ya vigezo vilivyozingatiwa kwa njia ya marekebisho ya viwango vilikuwa viwango vya maudhui ya unyevu, utolewaji rangi nafaka, mazao sumu, miongoni mwa mengineyo.

Baraza la Mazao la Afrika Mashariki (EAGC), kwa msaada kutoka kwa washirika wa Maendeleo pamoja na Mashirika ya Maendeleo ya Kimataifa, SIDA, USAID, DFID, CTA, miongoni mwao; yamekuwa yakishirikiana na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) katika mchakato wa kuimarisha viwango vya mazao ya nafaka,  mazao  ya jamii ya kunde, na mazao mengine tangu mwaka 2010 na Baraza limehamasisha na kujitolea rasilimali na ushirikishaji wadau katika mchakato huu.

Taarifa Zaidi  EA grain trade to intensify following standards harmonisation

Tanzania government eager to restore investor confidence

The Tanzania government has expressed its desire to kick start the mining industry and restore investor confidence.

This is according to ASX-listed rare earths junior Peak Resources and its CEO Rocky Smith who recently met with the Tanzania government to discuss the company’s Ngualla rare earths project.

“There is clear recognition by officials of the uncertainty that the announcement of the legislative changes created, and they are working pro-actively to demonstrate that Tanzania is still an attractive investment destination and open for business,” Smith says.

Smith also notes that Special Mining Licence (SML) applications will be given priority by the Mining Commission. The Ministry confirmed that Peak Resources’ SML application is one of only three current applications.

“We are extremely encouraged by our ongoing interactions with the Tanzanian government.”

Since the changes to the mining legislation in Tanzania in July this year Peak’s senior executives have spent considerable time in Tanzania continuing to develop the excellent relationship the company enjoys with the government and other stakeholders.

“The Mining Commission will assess project requirements on their own merits on a case by case basis. Early indications from the Ministry are that they understand that the export of the rare earth concentrate to Teesside is a practical requirement for the viability of the Ngualla project. Membership of the new Commission is expected to be announced by the end of the year.”

“These reassurances provide me with confidence that we can look forward to seeing some substantive progress on Ngualla’s final project development permitting in early 2018.”

More Info https://www.miningreview.com/news/tanzania-government-eager-restore-investor-confidence/

Huduma Zaidi / More Services

Muhunda Resources Limited inawatangazia wateja wake na wawekezaji wote kuwa inaendelea kutoa ushauri wa kifedha na kiuwekezaji katika ofisi zake za mjini Musoma.

Kampuni yetu hivi sasa imeongeza utoaji wa huduma zake za ushauri kwa kuongeza huduma za ushauri wa dhamana na hati-fungani za Serikali (Treasury Bills na Treasury Bonds) za Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kuongezea huduma zetu tunazotoa za ushauri wa kiuwekezaji katika Soko la Hisa la Dar es Salaam, DSE.

Gharama za ushauri zinazotozwa na kampuni yetu, Muhunda Resources Limited ni kuanzia shilingi elfu tano tu (5,000/-) za kitanzania.

Karibuni Nyote!

Muhunda Resources Limited informs its existing clients and investors that we are continuing to provide financial and investment advice at our Musoma offices.

Our company has now expanded its consulting services to include financial advice of Government Securities (Treasury Bills and Treasury Bonds)’ purchase that are offered through the Bank of Tanzania (BOT) in addition to our brokerage services for the Dar es Salaam Stock Exchange, DSE.

The advice cost charged by our company, Muhunda Resources Limited starts at Tanzania Shillings 5,000/- (about USD 2.25).

You are all welcome!

Barrick yakubaliana na Tanzania pia kutatua tatizo la kodi

Dar es Salaam/Toronto

Barrick Gold (ABX.TO) imesema Alhamisi hii kuwa kampuni inayoimiliki, Acacia Mining (ACAA.L) italipa dola za Marekani milioni 300 (paundi milioni 228.07 za Uingereza) na kugawana ‘faida za kiuchumi’ katika shughuli zake nchini Tanzania katika mpango wa makubaliano yaliyopendekezwa ili kutatua miezi miwili ya mgogoro wake na serikali ya Tanzania.

Mapema Alhamisi, Mwenyekiti wa Barrick, John Thornton aliuambia mkutano wa habari jijini Dar es Salaam kuwa kampuni hiyo imekubali kuilipa Tanzania dola za kimarekani milioni 300 kama ishara ya imani nzuri. Ilifafanua taarifa hiyo baadaye kuwa kampuni yake tanzu, Acacia itafanya malipo hayo.

Tanzania pia itapata sehemu ya asilimia 16 katika migodi mitatu ya dhahabu ya Acacia chini ya makubaliano hayo kwa mujibu wa Barrick na waziri wa serikali ya Tanzania. Acacia imesema imepokea nakala ya mpango wa makubaliano na itautolea ufafanuzi.

Thornton amesema makubaliano hayo yatahitaji idhini ya wanahisa huru wa bodi ya wakurugenzi wa Acacia. Bodi ya wanachama saba ya Acacia ina wakurugenzi wawili kutoka Barrick, mmoja kutoka Acacia na wakurugenzi huru wanne.

Serikali kutoka Indonesia hadi Afrika Kusini zinahitaji udhibiti mkubwa juu ya utajiri wa madini kwa jinsi bei za metali zinavyoongezeka. Baada ya kuhamia katika nchi zenye athari zaidi katika uchimbaji mpya, makampuni ya madini yanakabiliwa na kuongezeka kwa kile kinachoitwa utaifa wa rasilimali.

Barrick, kampuni kubwa duniani ya uchimbaji dhahabu inayomiliki asilimia 63.9 ya Acacia, ilianza mazungumzo na Tanzania mwezi Juni. Serikali ilipiga marufuku mauzo ya madini yasiyochakatwa na kutunga sheria mpya mapema mwaka 2017 ili kuongeza umiliki wa serikali katika migodi.

Acacia mwezi Julai ilipelekewa madai ya kodi za dola za kimarekani bilioni 190 kwa malimbikizo, adhabu na riba. Imekuwa ikituhumiwa na Tanzania kwa ukwepaji wa kodi kwa miaka kadhaa na pia kwa uthamini hafifu wa mauzo yake nje.

Ikiwa kampuni iliyosajiliwa kwenye soko la hisa la Uingereza, hisa za Acacia kwa siku ya Alhamisi zimefungwa zikiwa juu kwa asilimia 16 zikionyesha ahueni waliyopata wawekezaji wake katika makubaliano haya, wachambuzi walisema. Na hisa za Barrick zimefungwa zikiwa chini kwa senti 1 za Kanada kufikia dola za Kanada 20.15.

“Maelezo zaidi na ufafanuzi wa ziada unahitajika kuchunguza kikamilifu athari zake, lakini hadidu za makubaliano zinaonyesha kuwa na athari kidogo tofauti na matarajio,” alisema mchambuzi wa Masoko ya Hisa na Mitaji wa BMO,  Andrew Kaip katika taarifa yake ya Alhamisi.

Marufuku ya kusafirisha nje ilikuwa sehemu ya kushinikiza kwa ujenzi wa kinu cha uchenjuaji (smelter) nchini ili kufanya mauzo ya dhahabu ya nchi kuwa muhimu zaidi.

Rais John Magufuli hakusema kama marufuku ya kusafirisha nje ya nchi yataondolewa. Barrick na serikali itaunda kamati itakayofanyia kazi utatuzi wa madai ya kodi kwa Acacia.

“Kwa kuwa sisi sote ni wanahisa, tunaweza kukaa chini kwa kikombe cha kahawa na tukaamua masuala yoyote yaliyo bora,” Rais Magufuli alisema kwenye televisheni.

Pia aliamuru viongozi wa serikali kuanza mara moja majadiliano na wachimbaji wa almasi na tanzanite kufikia makubaliano kama hayo.

Tanzania ni wazalishaji wa dhahabu wa nne wa ukubwa barani na Acacia ni mchimbaji wake mkubwa zaidi.

Wiki iliyopita, Barrick ilisema uzalishaji wa robo ya tatu ya mwaka ulipungua kwa sababu ya masuala ya Tanzania.

Taarifa Zaidi: Barrick Gold, Tanzania reach partnership deal

“Rais Magufuli ni Kiongozi kwa wakati huu, nchini na barani”

  • Shirika lililosajiliwa Toronto, Tanzanian Royalty Exploration (CN: TNX) limemshukuru Rais John Magufuli, kwa kusema kuwa uwazi anaohitaji Rais katika sekta ya rasilimali, “ni wito ulio wazi kwa taratibu za pande zote kunufaika, na sio kutaifisha”.

Tanzania hivi karibuni ilipitisha sheria mpya zilizotungwa ili kuongeza mapato na kuipa uwezo serikali wa kufuta mikataba mibovu na kudhibiti usuluhishi wa kimataifa.

Mbali na sheria mpya, serikali imezuia mauzo ya makinikia ya dhahabu na shaba, ambapo uamuzi umesababisha kampuni ya Acacia Mining (LN: ACA) kutozwa malimbikizo ya kodi na penati zake mpaka kufikia dola za Kimarekani bilioni 190 katika migogoro na mchimbaji huyo, na mwezi uliopita ilitaifisha zaidi ya katati 70,000 za almasi kutoka mgodi wa Williamson unaomilikiwa kwa pamoja na Petra Diamonds (LN: PDL).

Hata hivyo Tanzanian Royalty Exploration, ambayo ina umiliki wa asilimia 45% ya mali na mapato ya mradi wa dhahabu wa Buckreef na serikali ya Tanzania, imesema kampuni zinazozalisha malighafi za madini zinapaswa kuwa na usawia katika kugawana mapato na serikali.

“Kama mfanyabiashara ninaefanya kazi nchini Tanzania kwa zaidi ya miaka 20, ni maoni yangu kwamba kufanya kazi kwa imani nzuri ni muhimu nchini Tanzania kama ilivyo kila mahali,” mwenyekiti mtendaji  huyo, James Sinclair alisema.

“Rais Magufuli ni Kiongozi kwa wakati huu, nchini na barani.”

Alisema kampuni hiyo haikuathiriwa na sheria mpya na anatoa maoni ya hivi karibuni kuhusu msemaji wa serikali, ambaye alisema hakuna ukweli katika ripoti zinazodai kwamba nchi ilikuwa na mikakati kutaifisha miliki za migodi.

Kampuni hiyo pia ilianza mazungumzo na serikali mwezi Julai ili kufadhili mradi wa kisasa gravity/CIL katika mgodi wa dhahabu wa wazi (open pit) wa Buckreef ambao una uwezo wa rasilimali zaidi ya ounces milioni 1 ardhini.

Kwa Taarifa Zaidi: “President Magufuli is a man for this time, country and continent”

Thamani ya Hisa za Kampuni ya Almasi, Petra Diamonds Zashuka baada ya Kukamatwa kwa Furushi la Almasi zenye Uthamini Hafifu

LONDON, Uingereza

Thamani ya hisa za kampuni ya Petra Diamonds zaanguka baada ya Serikali ya Tanzania kukamata furushi lenye vipande vya almasi zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 15 (takribani sh. bilioni 33) kama sehemu ya Uchunguzi wa Kamati ya Bunge katika madai ya uhalifu katika Sekta ya Almasi.

Kampuni hii iliyoorodheshwa kwenye Soko la Hisa na Dhamana la London imelazimika kufunga mgodi wake wa Williamson, chanzo cha mawe haya, kwa kuwa “wafanyakazi wake muhimu” wanasaidia mamlaka kwa uchunguzi kuangalia jinsi almasi zinavyothaminishwa.

Hisa za kampuni hiyo, ambayo inasema “haijapewa taarifa rasmi” za sababu ya uchunguzi, zimeanguka kwa karibu asilimia 25% wakati soko lilipofunguliwa, kabla ya kurejesha thamani kwa asilia 6% chini, chini ya senti za kiingereza 6.2p kufikia senti 83.75p.

Almasi zilikamatwa uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam tarehe 31 Agosti wakati zikitayarishwa kusafirishwa  kwa mauzo jijini Antwerp, na maafisa wa Tanzania wakidai kutothaminishwa ipasavyo.

“Wakati Kampuni Almasi ya Williamson katika nyaraka zake kuonyesha kwamba thamani ya almasi hizo ni dola za kimarekani milioni 14.798, uthamini mpya uliofanywa na serikali umeonyesha kuwa thamani halisi ya almasi hizo ni dola za kimarekani milioni 29.5,” ilisema taarifa ya Wizara ya Fedha.

“Miongoni mwa hatua za kisheria zitakazochukuliwa ni pamoja na kutaifishwa kwa almasi hizo zilizokamatwa baada ya kuthibitika kuwepo udanganyifu uliohusishwa katika kuonyesha thamani halisi ya madini hayo.”

Tanzania imeingia mtafaruku na makampuni kadhaa ya madini ya kigeni tangu uchaguzi wa 2015 wa John Magufuli, ambaye ni Rais anaejaribu kwa nchi kupata faida ya thamani itokanayo na mali ghafi.

Serikali yake juma lililopita iligundua “makosa” katika mchakato wa hisa za serikali katika Mgodi wa Williamson uliopunguzwa kutoka 50% hadi 25%, wakati pia Magufuli alishatoa agizo la uchunguzi juu ya madai ya uthaminishwaji wa chini kwa mauzo ya almasi nje.

Kampuni ya Petra inasema haijafahamishwa rasmi sababu za uchunguzi, ingawa ilitoa nyaraka kadhaa zinazohusiana na mchakato wa uthaminishwaji na malipo kwa serikali ya Tanzania.

Kampuni hiyo imesema kuwa usafirishaji wa karati za almasi 71,645 ulipewa thamani ya awali wa karibu dola milioni 14.8 na Shirika la Uthamini wa Almasi na Vito kabla ya kuandaliwa kwa kusafirishwa nje kwa mauzo.

Nyaraka za malipo ya mrabaha kwa serikali inaonyesha malipo ya karibu dola za kimarekani 888,000 pamoja na ada ya “ukaguzi na usafirishaji” ya karibu dola za kimarekani 150,000.

Kampuni hiyo pia imesema kuwa jumla ya malipo kwa serikali inategemea kile kilichopatikana kutokana na mauzo ya vito hivyo huko Antwerp, badala ya huo uthamini wa awali.

“Utaratibu wa ushindani wa wazi kwa kandarasi unaofanywa na kampuni ya Petra pia hutumiwa na makampuni mengine ya almasi na ina rekodi iliyothibitishwa ya uwazi katika bei,” kampuni hiyo ilisema.

“kampuni ya Petra ipo tayari kushirikiana na serikali ili kutatua suala hili na kuhakikisha kwamba taarifa sahihi zinapatikana kwa pande zote.”

“Kampuni itakuwa na fursa ya kuyashughulikia masuala mengine yote yaliyoibuliwa na matokeo ya Uchunguzi wa kamati ya Bunge mara itakapopokea nakala ya ripoti.”

Kampuni imesema shughuli za madini “zinafanyika kwa uwazi na kwa kufuata sheria kamili za Tanzania na Mchakato wa Makubaliano ya Kimberley”.

“Serikali ina fursa kamili ya uangalizi wa almasi zinazozalishwa katika mgodi, ambao hudhibitiwa na wawakilishi kadhaa wa serikali kwa kushirikiana na kampuni tangu hatua ya upatikanaji hadi hatua ya uuzwaji.”

Taarifa Zaidi:   Petra Diamonds market value falls after Tanzania seizes $15m shipment

 

CORE Securities Limited na Exim Bank kushirikiana katika Uwakala wa Hisa na Dhamana

DAR ES SALAAM, Tanzania

Biashara ya Hisa na Dhamana imechukua ukurasa mpya nchini baada ya Exim Bank na  Wakala wa Masoko ya Hisa na Dhamana, CORE Securities Limited kukamilisha mipango ya kuunganisha shughuli zao katika Masoko haya na sasa wakisubiria baraka za Tume ya Ushindani wa Biashara.

Muungano huu utazifanya kampuni hizi kuwa na uwezo mkubwa wa kiushindani katika Masoko ya Hisa na Dhamana kwa sababu ya Mtaji kuongezeka na matawi yaliyoenea vizuri kiushindani ndani na nje ya nchi.

Kwa mujibu wa Afisa Mtendaji Mkuu wa CORE Securities Limited, George Fumbuka, Exim Bank itanunua asilimia 80 ya kampuni ya CORE Securities ili kuimarisha uwezo wake wa kiushindani na kusambaza huduma zake kiurahisi.

“Ununuzi umezingatia masuala mawili. Kwanza ni mtaji mpya unaohitajika na pili ni mtandao mzuri wa matawi  – Exim ina yote hayo,” alisema.

Alisema hamu kubwa ni kufikia wateja wengi kote nchini na kwa kuunganisha na Benki ya Exim, wataongeza ufikishwaji wa huduma katika sehemu nyingi, ambayo ni karibu matawi 30 nchini na matawi mengine sita nchini Comoro, Djibouti na sasa Uganda.

Mkurugenzi Mtendaji alisema kuwa Uwakala wa Masoko ya Hisa na Dhamana umebadilika ambapo kwa sasa Mawakala sio tu watoa huduma, bali pia hununua Hisa za Awali (IPO) na kuziuza mara thamani inapoongezeka. Alisema kuwa hicho ndicho kilichotokea wakati wa IPO ya Vodacom ambapo karibu asilimia 95 ya hisa zote zilinunuliwa na taasisi na hasa Mawakala wa kigeni wa Masoko ya Hisa na Dhamana.

“Tunahitaji mfuko wa ziada ili kuwezesha kununua hisa wakati wa IPO … na pia ada ya leseni imepanda kwa siku za hivi karibuni,” Bwana Fumbuka, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Mshindi wa Tuzo ya Wakala Bora Afrika Mashariki mwaka 2013 alisema.

Kwa mujibu wake, hapo awali kuwa Wakala wa Masoko ya Hisa na Dhamana zilihijitajika shilingi milioni 20 lakini leo zinahitajika dola za kimarekani 500,000 takribani shilingi bilioni 1.10. Kiwango cha Tanzania ni cha chini ikilinganishwa na Kenya dola za Kimarekani 800,000 (1.2 bilioni), Nigeria dola za kimarekani milioni 1.0 (2.2 bilioni) na Afrika Kusini dola za kimarekani milioni 2.0  (4.4 bilioni).

Hata hivyo, mpango mzima haujajulikana bado na hautaweza kupita bila kupata baraka za Tume ya Ushindani (FCC). FCC jana ilitoa idhini ya umma kutoa maoni ya wadau kuhusu ushirikiano huu.

“FCC kwa sasa inachunguza ushirikiano unaotarajiwa kulingana na  Sheria ya Ushindani ya mwaka 2003 na Kanuni za Ushindani za mwaka 2013,” ilisema taarifa hiyo.

Taarifa Zaidi: Dar bank plans to buy stock brokerage firm

 

Wawekezaji wa Nje Waruhusiwa kununua Hisa za Awali (IPO) kwenye Kampuni za Mawasiliano

Serikali kupitia Mapendekezo ya Sheria za Kifedha (Finance Bill 2017) imeruhusu wawekezaji wa kigeni kushiriki katika ununuzi wa hisa za awali (IPO) katika sekta ya mawasiliano, mdhibiti wa masoko ya hisa na mitaji alisema, Ijumaa.

Ruhusa hii inawawezesha wageni kushiriki pia katika hisa za awali (IPO) za Vodacom Tanzania Plc, kampuni tanzu ya Vodacom Group ya Afrika Kusini.

IPO ya Vodacom ilizinduliwa mwezi Machi na ilifunguliwa tu kwa wawekezaji wa ndani, lakini awali haikufanya vyema kutokana na hisia za ukwasi katika soko la ndani na kuongezewa muda.

 

Tanzania lifts ban on foreigners investing in telecom IPOs

Tanzania has lifted the banning on foreign investors participating in initial public offerings in the telecoms sector, the capital markets regulator said on Friday.

The removal of the restriction allows foreigners to take part in the IPO of Vodacom Tanzania Plc, a subsidiary of South Africa’s Vodacom Group.

The Vodacom IPO was launched in March and initially only open to local investors, but take-up has been sluggish amid concerns over adequate liquidity in the local market.

More Details

Govt amends law to allow access to IPOs

DODOMA, Tanzania

In an unprecedented move, the government is amending the Electronic and Postal Communication Act (Epoca) 2010 with a view to allowing diverse investors take part in Initial Public Offerings (IPOs) for Telecommunication companies.

The Act, which was amended in the Finance Act, 2016 requires telecommunication companies to offload 25 per cent of their shares to Tanzanians only via IPOs and so far, it is only Vodacom Tanzania Public Limited Company (PLC) that has completed the IPO process though, it has remained mum on the outcome.

More Details

Barrick Agrees to Pay Money Owed to Government

Barrick Gold Corp. Chairman John Thornton met Tanzanian President John Magufuli on Wednesday and said his company is willing to pay money owed to the East African nation.
Shares in subsidiary Acacia Mining Plc surged as much as 11 percent.

“Thornton said his company is ready to hold talks with Tanzania that will consider the interests of both sides and is ready to pay all the money it’s expected to pay Tanzania,” Magufuli’s office said in an emailed statement from Dar es Salaam, the commercial capital.

The meeting took place two days after the Tanzanian leader accused Acacia Mining of operating illegally and demanded it pay unpaid taxes. The accusation came after a committee carried out an audit of the country’s mineral exports over the past 19 years.

Barrick, which owns 64 percent of Acacia, will help Tanzania build a smelter, according to the presidency’s statement.

Giles Blackham, a spokesman for Acacia Mining, didn’t immediately respond to an emailed request for comment.

More on Barrick/Acacia